×

SPOTI HAUSI LIVE: Kwa Mwendo Huu, Yanga Hawafiki Popote


KIPINDI cha Spoti Hausi leo Alhamisi kipo hewani kuanzia saa 10:00 jioni ambapo wanachambuzi wako watakuchambulia kilichosababisha timu za Simba na Yanga kuondolewa mapema kwenye michuano ya kimataifa.

 

Kupitia Spoti Hausi kinachodhaminiwa na Kampuni ya TECNO Mobile Ltd, kinakuletea uchambuzi wa kama Yanga wanaweza kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, wapi watakwama na wapi watakuwa na nafasi nzuri ya kuwika? Usikose leo saa kumi kamili jioni.

 

Pia, mshindi wa Shindano la #BeatsByDre kutoka Gazeti la #SpotiXtra linalotoka kila Jumapili atatangazwa leo kupitia droo maalum itakayochezeshwa kwenye Kipindi cha #SpotiHausi SAA 10:00 jioni kupitia #GlobalTVOnline.

 

Washindi wengine watakaotangazwa ni wawili ambao watajinyakulia jezi za vilabu vya Ligi Kuu ya England.