×

Polisi: Vijana Walikuwa 3 Wakampiga Risasi Kifuani, Walitoroka Hawakuchukua Chochote – Video

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limesema kuwa linachunguza tukio la mauaji ya Christina Nimrod Nindi (56) Mngoni, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo na mkazi wa Kitongoji cha Banawanu, Kijiji cha Ugwachanya katika Kata ya Mseke Tarafa ya Mlolo.

Nindi alifariki dunia Novemba 12, 2024 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Tosamaganga baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi kifuani pamoja na kupigwa na kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu alivamiwa na vijana watatu wasiofahamika katika nyumba anayoishi na binti zake wawili.

Pia watu hao walimshambulia binti mmoja wa marehemu na kumuumiza usoni pamoja na jirani yake ambaye naye ameumizwa eneo la ubavu wa kushoto kwa kupigwa na kitu butu alipokwenda kutoa msaada baada ya kusikia kelele kutoka kwa binti wa marehemu.

Leave a Comment