×

Huu Moshi Wa Wambura Kufungiwa Utazamwe Kwa Umakini

MCHEZO wa soka ni biashara kubwa katika mataifa mengi duniani, kuna wachezaji ambao wanalipwa mishahara mikubwa na malipo mengine ya matan­gazo ya biashara kutokana na vipaji vyao kwenye mchezo huo.

 

Tanzania tupo katika njia nzuri ya kuelekea katika mafanikio an­galau ya kuwa nchi iliyoonyesha mfano wa kuwa na ramani nzuri ya soka, na hiyo inachangiwa na sisi wenyewe kukosoana na kuwa wazi pindi tunapoona kuna mambo hayaendi sawa.

 

Wakati hali ikiwa hivyo, kumean­za kufukuta mvutano wa ndani ya Shirikisho la Soka la Tanza­nia (TFF) baada ya maamuzi ya kufungiwa maisha kwa Michael Wambura ambaye alikuwa Kai­mu rais wa taasisi hiyo kubwa ya mchezo wa soka.

 

Inaweza kuonekana ni kitu kido­go lakini kitendo cha Wambura ambaye alichaguliwa kwa kura nyingi kufungiwa baada ya tuhu­ma zake kuibuliwa ndani ya muda mfupi, kinaweza kusababisha maswali mengi.

 

Hoja ni kuwa Wambura kafungi­wa kwa makosa yake ya nyuma, imani ya wapiga kura juu yake inaonekana ilikuwa kubwa na ndiyo maana hata ushindi wake ukawa mkubwa, kuondolewa kwake hakuwezi kuchukuliwa kawaida kwa mazingira hayo.

 

Licha ya kuwa Rais wa TFF, Wal­lace Karia hakuwa tayari kuli­zungumzia hilo kwa madai kuwa bado lipo katika mikono ya kamati zenye mamlaka, ni vema uongozi mzima wa TFF ukatazama suala hilo kwa ji­cho la tatu ili lisije likachangia kuwavuruga wanachama wao na mwisho wake kusababisha mgogoro ni mbaya
kwa afya ya mchezo huo.

Na: Bodi ya Uhariri/Maoni Ya Championi