
Kumbukumbu ya wafanyakazi na mafundi wa kichina wapatao 65 waliopoteza maisha wakiwa katika ardhi ya Afrika wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara, yamefanyika katika makaburi maalumu yaliyopo Gongo la Mboto.
Akizungumza na vyombo vya habari balozi wa China nchini Wang Ke,alisema kuwa anatoa shukurani za dhati kwa kwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariku Dk.Augustine Mahiga,na viongozi wote kwa kuhudhuria na kuungana katika siku hiyo muhimu wa utamaduni wa kichina Qingming.
Balozi huyo aliongeza kuwa naomba urafiki ambao huo karibia nusu karne sasa uendele hivyohivyo kwa maana ujenzi wa Reli ya Tazara ulitumia miaka 6 kumalizika wenye urefu wa wa kilometa 1860.3



