×

WAJUE MABEKI WENYE MABAO MENGI ZAIDI UEFA

GERARD Piqué sasa ni beki anayekamata nam­ba tatu (pacha) kwa ku­funga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bao lake al­iloifungia Bar­celona dhidi ya Roma, lilikuwa la 12 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kumpeleka hadi namba tatu pacha katika orodha ya mabeki wal­iofunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Piqué aliiwezesha Bar­celona kushinda mabao 3-0 ka­tika mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Roma Juma­tano iliyopita .

HAWA NDIYO MABEKI WAFUNGAJI BORA ZAIDI WA WAKATI WOTE UEFA:

Roberto Carlos 16

Iván Helguera 15

Dani Alves 12

Gerard Piqué 12

Christian Panucci 11

Sergio Ramos 11