×

Shabiby: Nondo Ana Umaarufu Gani, Mnachafua Serikali tu! – VIDEO

Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby, amesema hakuna umuhimu mamlaka za serikali kutumia vyombo vya abari kuwaita baadhi ya watu kwa ajili ya kuwahoji kutokana na tuhuma wanazokabiliwa nazo.

 

Shabiby amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma leo Aprili 12, 2018  huku akitolea mfano tukio la Mwenyekiti wa TSNP ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu (UDSM), Abdul Nondo, ambaye aliitwa na Mamlaka ya Uhamiaji kwa ajili ya kuhojiwa uraia wake, na kusema kwamba vitendo hivyo vinaichafua serikali kwa kaisi kikubwa.

 

“Sasa hivi kuna watu kwenye Utumishi ambao wanafanya mambo ya kuichafua Serikali ya CCM, kulikuwa na haja gani ya kumita yule kijana Abdul Nondo kumhoji sijui alete cheti cha kuzaliwa cha bibi cheti cha mjomba, cheti cha babu? Mamlaka inshindwaje kufanya investigations zake (uchunguzi) ili kubaini ukweli mapaka iite wanahabari?

 

“Tunawapa watu umaarufu wakati kesi ipo polisi, ipo mahakamani, kuna watu wengine watatumia hiyo kitu kusema Serikali ya CCM ikimtaka mtu inamuomba uraia wake, sidhani kama Serikali ina haja mtu mdogo kama yule ambaye hata hana madhara yoyote,” alisema Shabiby.

 

MSIKIE SHABIBY AKIZUNGUMZA