KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amekiri kuwa kuna wachezaji ambao watalazimika kuondoka klabuni hapo kwa kutofikia levo za kuichezea timu hiyo inayomiliki Uwanja wa Old Trafford.
Inajulikana wazi kuwa Mourinho atafanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake ili kuweza kuwania ubingwa wa Premier League ambao msimu huu umeenda kwa wapinzani wao wa jiji moja, Manchester City.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, amekuwa akiwakosoa Anthony Martial na Luke Shaw kwa kutocheza katika ubora anaoutaka huku uhusiano wake na Paul Pogba ukielezwa kuwa upo katika utata.
“Tunahitaji watu ambao watakuwa na mwendelezo mzuri uwanjani, tunataka watu ambao wataondoa tofauti iliyopo kati yetu na City.
“Najua kuna wachezaji watakaofikia kiwango ninachotaka na wengine hawatafika, ninalijua hilo.
“Unapofungwa na timu z i l i zopa nda daraja, kisha ukazifunga timu kubwa siyo dalili nzuri kwangu,” alisema Mourinho.
Comments are closed.