CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha habari zilizoenea kwamba Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, amejiuzulu.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, aliyekuwa akiongea na mtangazaji wa Global TV Online leo, kiongozi huyo hajajiuzulu na kwamba habari zilizoenea kuhusu jambo hilo si za kweli.
Kwa takribani siku mbili sasa kumekuwepo taarifa zisizo rasmi katika mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuhusiana na kile kilichodaiwa kuwa Kinana ameandika barua ya kujizulu wadhifa huo.