×

SENEGAL HATARI, YAWAPIGA POLAND

SENEGAL imekuwa timu ya kwanza kuwatoa kimasomaso Waafrika baada ya jana Jumanne kuichapa Poland mabao 2-1, kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia. Senegal walionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo huo huku wakionyesha nidhamu ya hali ya juu kwa dakika zote tisini. Senegal walifanikiwa kujipatia bao lao katika dakika ya 37, baada ya Thiago Cionek kujifunga wakati akijaribu kuokoa shuti la Idrissa Gueye.

Baada ya bao hilo, Senegal walitulia na kucheza kwa kujihami sana huku mabeki wao wakifanya kazi kubwa sana kumzia Robert Lewandowski ambaye alikuwa akiingia kwenye eneo la hatari la timu hiyo mara kwa mara. K i p i n d i cha pili, Senegal waliendelea kucheza kwa umakini mkubwa na kufanikiwa kujipatia bao la pili katika dakika ya 59, baada ya Mbaye Niang, kuiwahi pasi ya nyuma iliyopigwa na kumchambua kipa wa Poland, Wojciech Szcesny.

Poland walifanikiwa kusawazisha bao moja kupitia kwa mshambuliaji wao Grzegorz Krychowiak aliyefunga kwa kichwa huku mabeki wa Senegal wakiwa wamezubaa.

 

Senegal imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kupata ushindi kwenye Kombe la Dunia mwaka huu, kwenye mchezo wa kwanza baada ya Misri, Nigeria, Morocco na Tunisia kupoteza michezo yao. Hii ina maana kuwa hawa wana nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya 16 Bora kama watafanikiwa kushinda mchezo mmoja tu kwenye Kundi H, ambalo pia lina timu za Japan na Colombia.

Katika mchezo wa kwanza, Colombia walianguka baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Japan kwenye mchezo mwingine uliokuwa mkali na wa kuvutia. Colombia walipata pigo katika dakika ya tatu tu baada ya Carlos Sanchez kupewa kadi nyekundu. Shinji Kagawa na Keisuke Honda huku Colombia wakifunga bao lao pekee kupitia kwa Juan Qintero kwa mkwaju wa faulo.

MATCH FACTS
Poland (4-3-2-1): Szczesny 4, Piszczek 5.5 (Bereszynski 81, 6), Pazdan 6, Cionek 5, Rybus 5.5, Blaszczykowski 5 (Bednarek 45, 5), Krychowiak 6, Zielinski 6, Grosicki 6, Milik 6.5 (Kownacki 73, 6), Lewandowski 6

Unused subs: Jedrzejczyk, Goralski, Linetty, Bialkowski, Teodorczyk, Glik, Peszko, Kurzawa, Fabianski

Goal: Krychowiak 86

Booking: Krychowiak 12

Senegal (4-4-2): K N’Diaye 6.5, Sabaly, 7 Koulibaly 8, Sané 7.5, Wague 7, Gueye 7, A. N’Diaye 7 (Kouyate 88), Diouf 7 (Ndoye 60, 6.5), Mané 6.5, Sarr 7, Niang 7.5 (Konate 74, 6)

Unused subs: Diallo, Mbengue, Mbodji, Sow, Kouyate, Konate, Sakho, B. N’Diaye, Balde, Gassama, Gomis

Goals: Cionek og 37, Niang 61

Bookings: Sane 49, Gueye 72

Referee: Nawaf Shukralla (BHR) 7

Star Man: Kalidou Koulibaly