USIKU wa kuamkia jana ulikuwa ni wa raha yake na wa kihistoria kwa msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja na mkewe ambaye ni muigizaji wa Bonbgo Movies, Irene Uwoya baada tajiri mmoja jijini Arusha kuibuka na kuwazawadia kiwanja ambacho watajenga nyumba yao ya kuishi jijini humo.
Tukio hilo lilifanyika katika ukumbi wa Tripple A wakati wa hafla ya fainali za shindano la kusaka vipaji vya kuimba lililoandaliwa na kampuni ya Kismaty Media, alipokuwa ameenda kwa ajili ya kukabidhi zawadi kwa washindi.