×

MUNA LOVE: BABA WA PATRICK NI CASTO, NITAMUABISHA PETER

KUFUATIA kifo cha mtoto wa Muna Love, Patrick aliyeaga dunia jana nchini Kenya akipatiwa matibabu, taarifa zenye mkanganyiko zimekuwa zikisambaa mitandaoni kuhusu nani ni baba halisi wa mtoto huyo huku wengine wakisema ni Casto na wengine wakidai ni ndugu Peter Zacharia.

 

Global TV Online ilifunga safari mpaka Mwananyamala nyumbani kwa Peter Zacharia Komu anayedai kuwa ni mume wa ndoa wa Muna na ndiye baba mzazi wa marehemu Patrick huku akieleza kuwa amekuwa akimhudumia mtoto huyo kuanzia matibabu yote, matunzo na ada ya shule na kueleza kuwa Casto si baba wa mtoto huyo kama watu wanavyopotoshwa.

Alichokisema  mama wa mtoto msanii wa Filamu za Bongo na mdau wa Muziki wa Bongo Fleva, Rose Alphonce ‘Muna Love’ kupitia page yake ya Instagram;-

“Jaman jamani 😭😭😭😭😭😭 naomba nimzike mtoto wangu 😭😭😭😭 vaeni viatu vyangu. Kuna siri kumbwa amjawahi kuijua nawaomba nimzike mtoto wangu alafu ndiyo mnitukane. Mimi 😭😭😭😭😭😭 naumia jamani, namuheshimu Peter siwezi kuweka kitu hapa maana nitamwaibisha….

 

Siwezi kumsema Casto maana yeye anajua wapi alikosea, nawaombeni jamani, naomba nataka kumzika mwanangu. Miaka miwili nahangaika na Paty wangu 😭😭😭😭😭😭😭😭, nimalize kumzika niongee.

Nnyiwe wanawake mnaonihumuku, vaeni viatu vya siri nilizohifadhi… baba wa mtoto ni Casto, inatosha 😭😭😭😭😭😭😭😭, nitukaneni mimi nife ila Paty ni kiongozi alieniongoza nione maisha mapya na nimjue Mungu… Nitalia milele mimi.

 

Paty wangu😭😭😭😭😭😭😭😭leo wanakugombania mwaanangu, natamani urudi mara moja😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭… Mwanangu ntaleta ijumaa na ntamzika Jumamosi😭😭😭😭😭, msiba uko kwangu Mbezi Beach.” amesema Muna.

Aidha, Dada wa Muna naye amefunguka na kubainisha kuwa familia inafahamu mtoto huyo ni wa Peter na siyo Casto. Kupata mengi zaidi, fuatilia mahojiano hayo kupitia YouTube ya Global TV Online.

 

VIDEO: Baba Halisi wa Patrick Afunguka Mazito, Kifo cha Mwanaye