×

Wanne Wafariki kwa Ajali Tatu Tofauti Dar

Watu wanne wamefariki dunia papo hapo katika ajali tatu tofauti zilizotokea ndani ya muda usiozidi saa mbili katika barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, Julai 6, 2018.

 

1. Ajali ya kwanza.

Katika ajali ya kwanza iliyotokea Tabata Dampo mwenda kwa miguu mmoja aliyekuwa akivuka katika alama za Pundamilia amefariki papo hapo baada ya kugongwa lori (Semi trailer) na kisha lori hilo kupinduka.

Inadaiwa mwenda kwa miguu huyo aliliona Lori hilo likija kwa kasi lakini alistuka na kusimama akaashiria lisimame lakini halikusimama na kumgonga na kumtupa katika kituo cha mafuta cha Puma

2. Ajali ya pili.

Katika ajali ya pili inadaiwa kuwa Mwenda kwa miguu alikuwa akivuka barabara kwa kuangalia magari ya upande mmoja tu yanayotoka Ubungo na hivyo kugongwa na kufariki papo hapo na gari lililokuwa linatokea Buguruni.

3. Ajali ya tatu

Aidha, katika ajali ya tatu iliyotokea maeneo ya darajani katika mto Msimbazi inadaiwa kuwa watu wawili waliokuwa wamepakiwa mshkaki kwenye bodaboda wamegongwa na kufariki papo hapo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi bado halijathibitisha taafa hizo.