MUDA mfupi baada ya mwili wa mwanaye kuletwa nyumbani kutoka chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, mama mzazi wa marehemu Patrick, Muna Love, asubuhi ya leo amelazwa ghafla katika Hospitali ya Aga Khan kwa kuzidiwa na homa.

Mwili ulipelekwa moja kwa moja hadi nyumbani kwa baba wa mtoto, Peter Zacharia, maeneo ya Mwananyamala kwa ajili ya kuagwa.

Baada ya kuuona mwili wa mwanaye, Zacharia alishindwa kujizuia na kujikuta akilia kwa uchungu.
Hadi tunakwenda mitamboni, mwili huo ulikuwa umeshaagwa nyumbani na tayari ulikuwa umepelekwa katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni, kwa ajili kuagwa.