×

Hatimaye Ronaldo Afanya Vipimo Juventus

HUKU  shamra za fainali ya Kombe la Dunia baina ya Ufaransa na Croatia zikiwa zinaendelea kusikika duniani, masikio na macho ya wapenzi wa soka duniani yameanza kuhamia katika kuwasili kwa nyota wa mchezo huo duniani, Cristiano Ronaldo jijini Turin kujiunga na timu ya Juventus akitokea katika timu ya Real Madrid.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 33, amewasili katika timu hiyo na kufanyiwa vipimo mbalimbali ambapo yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake kwenda timu hiyo ya Italia, akiwa ameondoka Real Madrid ya Hispania aliyoitumikia kwa miaka tisa na kuipatia ubingwa wa ligi ya nchi hiyo mara nne.

 

Kitita cha uhamisho wake ni Paundi milioni 88 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 665.6 za Tanzania.

Mashabiki wa Juventus wamejitokeza kwa wingi mapema leo kumpokea nyota huyo.