The House of Favourite Newspapers

Okwi Aanze Na Kagere

LAUDIT Mavugo ambaye msimu uliopita aliichezea Simba, amepata taarifa kuwa timu hiyo imemsajili Meddie Kagere hivyo kwa hali ilivyo ni vyema John Bocco akaanzia benchi na kuwapisha Kagere na Emmanuel Okwi kikosi cha kwanza.

 

Mavugo ambaye msimu uliopita aliifungia Simba mabao manne kwenye ligi, alisema anamfahamu sana Kagere na aliwahi kucheza naye katika klabu ya Polisi Rwanda hivyo hakuna mtu wa kumdanganya kuhusu uwezo wake.

 

“Nimesikia Kagere amesaini Simba, kwangu ni mchezaji mzuri ambaye anajua kufunga kwa sababu nilishawahi kucheza naye kwenye timu moja ya Polisi Rwanda na alikuwa anafunga sana, nadhani atakuwa msaada mkubwa kwao katika michuano ya kimataifa.

 

“Binafsi naona ni vizuri kocha akamuanzisha pamoja na Okwi kwa kuwa wote ni wafungaji wazuri, siyo kwamba Bocco hawezi, hapana ila naona kama Bocco akitokea benchi itakuwa vizuri kwao lakini Kagere aanze na Okwi halafu waone kitakachotokea,” alisema Mavugo ambaye ni mchezaji kipenzi wa Haji Manara anayemuita King Mavugo.

Comments are closed.