×

UICHOKIJUA KUHUSU NIKKI WA PILI KUWANIA URAIS WA TANZANIA

Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo kutoka Kampuni ya Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ hivi karibuni amezua gumzo baada ya kuweka wazi kupitia Mtandao wa Kijamii wa Twitter kwamba ana ndoto ya kuwania Urais wa Tanzania.

Baada ya kutupia posti hiyo, mashabiki wengi waliibuka na kudai anatatufa kiki, lakini akizungumza na Risasi Vibes, Nikki wa Pili alianika kwamba siyo kiki bali ni kweli ana mpango wa kuwania Urais wa Tanzania.

“Watu wanaweza kufikiri kwamba ninatafuta kiki, lakini ukweli ni kwamba ni ndoto yangu siku moja kuwa Rais wa Tanzania. Kwa sasa ninasogeza umri, baada ya mwaka 2025, nitafahamu ni chama gani kitanipa tiketi.

“Kuhusu nafasi hii ‘CV’ yangu inajieleza na namna ambavyo watu wananiamini, nitaendelea kufanya mambo ya kujenga uaminifu zaidi ili baadaye niwatumikie Watanzania,” alisema Nikki.

SHAMUMA AWADHI