
Kikosi cha Yanga kikiwa na wachezaji 18 kimewasili salama nchini Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports utaochezwa Jumatano kesho.

Yanga itashuka dimbani ikiwa haina matumaini ya kuendelea na mshindano hayo zaidi tu ya kusaka heshima pekee baada ya kutokana na kutokuwa na nafasi tena ya kusonga mbele kwenye kundi D.
Katika Kundi hilo Yanga mpaka sasa imekalia mkiani ikiwa na alama 4 pekee huku Gor Mahia wakiwa nafasi ya kwanza, USM Alger wakishika namba mbili na Rayon wakiwa nafasi ya tatu.
