×

Hofu Mauaji ya Albino Yaongezeka Kuelekea Uchaguzi wa 2020 – Video

HOFU ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini inadaiwa kuongezeka hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

 

Hayo yamesemwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LRCH) leo wakati wakizindua ripoti yao ya nusu mwaka kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu iliyojikita katika maeneo matatu ambayo ni haki za kiraia na kisiasa, haki za kijamii, haki za makundi maalum ikiwemo walemavu, wanawake na watoto.

 

“Matukio ya ukatili kwa wanawake yameongezeka ikilinganishwa na mwaka jana, kwa kipindi cha kuanzia Januari 2018 hadi Juni 2018, idadi ya wanawake 1,218 wameripotiwa kubakwa, inakadiriwa ni wanawake 203 kila mwezi.

 

“Matukio ya kujichukulia sheria mkononi na mauaji ya kwa imani za kishirikina yamepungua kutoka 172 hadi 106. Hofu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi imeongezeka kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 lakini hakuna tukio la mauaji lililoripotiwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu.

“Licha ya jeshi la polisi kutotoa ripoti, lakini vyombo vya habari viliripoti mauaji yaliyosababishwa na jeshi hilo ikiwemo mauaji ya mwanafunzi Akwilina Akwilini. Sera ya serikali ya elimu bure imesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi walioandikishwa mashuleni, lakini kuna changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa matundu ya vyoo,” imesema Ripoti hiyo.

 

VIDEO: FUATILIA RIPOTI HIYO HAPA