The House of Favourite Newspapers

LYNN ABANWA KUMPIKU MOBETO KWA MONDI

Irene Godfrey ‘Lynn’

MUUZA nyago (video queen) aliyewahi kuuza sura kwenye Wimbo wa Kwetu wa Msanii Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Irene Godfrey ‘Lynn’ amebanwa na kupata kigugumizi baada ya kuulizwa kuhusu uhusiano wake na Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.  Ubuyu uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ukiambatanishwa na picha ulidai kwamba wawili hao walikuwa pamoja visiwani Zanzibar kwa ajili ya mapumziko huku Lynn akidaiwa kumpiku mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa Diamond. Fununu juu ya uhusiano wa wawili hao zilianza kusambaa baada ya Lynn kushuti video na Rayvanny mwaka juzi, lakini uthibitisho wa tetesi hizo haukupatikana.

Ilidaiwa kwamba, awamu hii wawili hao wameamua kuyaweka wazi mapenzi yao na huenda Lynn akachukua nafasi ya Mobeto ambaye alifanikiwa kuzaa mtoto mmoja na Diamond. Baada ya picha hizo ‘kusumbua’ mitandaoni, Ijumaa lilimtafuta mwanadada huyo na kumbana ili kupata undani wake na Diamond kama wapo kwenye uhusiano au walikwenda kwa ishu ya kikazi, lakini aliishia kutoa povu kwa mwandishi wetu. “Nini? Bwana? Mi’ sijui, mniache na maisha yangu, tena mniache,” alijibu Lynn kwa kifupi huku akisitasita kisha akakata simu baada ya kugoma kutoa ushirikiano. Kwa upande wake Diamond alipotafutwa na gazeti hili ili kueleza mbivu na mbichi kati yake na Lynn alifunguka;

“Kwa nini kila mwanamke nahusishwa naye? Tatizo kila mrembo ninayekuwa naye karibu kikazi watu wanasema natembea naye. Hakuna chochote kati yangu na huyo Lynn zaidi ya kufahamiana naye kikazi. “Kuna wakati napata ugumu sana maana kila mwanamke ninahusishwa naye wakati hata sijawahi kumtamkia neno la mapenzi zaidi ya kazi tu. “Unajua kazi yangu ni muziki so (hivyo) kukutana au kuwa karibu na warembo ni sehemu ya kazi yangu, sasa watu wakiniona nao wanajua tayari niko nao kimapenzi

STORI: Shamuma Awadhi, Risasi Jumamosi

Comments are closed.