×

SPOTI XTRA LAENDELEA KUKIMBIZA SOKONI

Ofisa wa Usambazaji wa Magazeti ya Global, Anthony Adam (kulia) akiwaelekeza madereva wa daladala wa Tandika jinsi ya kujishindia zawadi mbalimbali kupitia shindano lililopo kwenye gazeti hilo.

GAZETI  jipya na bora la michezo la Spoti Xtra leo limeendelea kukimbiza mitaani ambapo wasomaji kwenye kona mbalimbali za Jiji la Dar wameonekana kulichangamkia.

Maofisa wa Global wakiweka bango la Spoti Xtra kwenye meza ya mmoja wa wauza magazeti wa Tandika Sokoni.

Kikosi cha mauzo na usambazaji leo kilitembelea maeneo ya Buguruni, Temeke-Mwisho, Tandika-Maguruwe, Mwembe-Yanga, Temeke-Mikoroshini ambapo sehemu zote hizo walinaswa wasomaji wakiwa bize na Spoti Xtra.

Mmoja wa maofisa wa Global akimuelekeza jambo msomaji huyu aliyekutwa Tandika Mwembe-Yanga.
Ofisa wa Global (katikati) akiwasisitiza wasomaji kushiriki shindano lililopo kwenye gazeti la Spoti Xtra baada ya kuwakuta Tandika-Maguruwe wakijisomea gazeti hilo.
Wasomaji wa Temeke-Mikoroshini  wakipata burudani ndani ya Spoti Xtra.
Wasomaji wa Temeke-Mwisho wakilifuatilia jinsi ya kushiriki shindano linaloendeshwa kwenye gazeti la Spoti Xtra pamoja na uhondo mwingine uliomo.
Ofisa wa Spoti Xtra akiwaelekeza jambo wasomaji waliokutwa Mtoni Kwa Azizi Ally wakisoma Spoti Xtra.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL