×

Kibu Denis, Dilunga Majanga Simba

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefungukia maendeleo ya wachezaji wao Kibu
Denis na Hassan Dilunga
ambao kwa sasa ni majeruhi.


Hiyo ni katika kuelekea
mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas utakaochezwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Ally amesema: “Leo (jana) asubuhi Dilunga ameenda kuangaliwa tatizo
lake na kujua ni kwa muda
gani atakaa nje ya uwanja.

 

“Kwa upande wa Kibu, yeye bado hali yake siyo nzuri, ila Taddeo Lwanga amesharejea na kuanza
mazoezi na timu na huenda
mwalimu akamtumia katika mchezo wa Jumapili.”

Leave a Comment