×

MAOFISA USTAWI WA JAMII WAPIGWA MSASA KUHUSU UALBINO

Maofisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji jana walihudhuria mafunzo ya uelewa kuhusu ualbino na elimu ya Amani na maadili iliyotolewa na mradi wa Haki Yetu mkoani Kigoma.

 

Mradi huo umekua ukiendeshwa tokea Aprili mwaka huu katika Mikoa ya Kigoma na maeneo ya jirani kwa ushirika wa wadau mbalimbali lengo lao likiwa ni kutoa msaada kwa jamii kuelewa zaidi kuhusu ualbino, kupunguza imani potofu, kuwajengea watu wenye ualbino misingi ya kujiamini ualbino pamoja na kutengeneza jamii shirikishi isiyokuwa na ubaguzi wa aina yoyote kwa watu wenye ualbino.

Katika mradi hu0, misingi muhimu ambayo imekua ikiwekewa msisitizo ni pamoja na kuzingatia utu, kuwapa nafasi watu wenye ualbino bila kuwabagua, kushirikiana nao kwenye masuala ya elimu na uchumi lengo likiwa ni kujenga Taifa bora.

Mradi wa Haki Yetu unatekelezwa na Mashirika ya Under The Same Sun, CEFA Tanzania na GNRC Tanzania, ukilenga kuelimisha jamii kuhusiana na ualbino.