
INASIKITISHA! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia historia ya maisha ya Hamis Salum maarufu kwa jina la Best, ambaye yu mgonjwa wa matatizo ya akili.
Kaka wa Hamis aitwaye Shaban amezungumza na Global TV na kuzungumzia suala la ugonjwa wa mdogo wake ambaye maisha yake ni ya shida kutokana na matatizo yake ambayo ameyapata akiwa mtu mzima.
Fuatilia kwa kina Mahojiano haya ili ufahamu alianzaje kuugua, anaishije, ni changamoto zipi anazipitia. Iwapo ukiguswa uweze kutoa msaada kwa kupitia nambari 0712 – 32 12 82.