KOCHA wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema kama mshambuliaji wake, Mrundi, Amissi Tambwe anataka kucheza kikosi cha kwanza basi ni lazima ‘akaze’ ili afi kie kiwango cha straika wa Simba, Meddie Kagere.
Tambwe ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora mara mbili katika Ligi Kuu Bara akiwa na Simba na Yanga, hivi karibuni alirejea uwanjani kwa kasi na kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United. Mrundi huyo tangu amerejea kikosini amekuwa hana nafasi ya kudumu kutokana na majeraha ya goti ambayo yalianza kumuandama tangu msimu uliopita.
Zahera alisema hana hofu na kiwango cha Tambwe lakini kwa sasa kiwango chake kimeshuka kikisababishwa na majeraha ya mara kwa mara. Zahera alisema, Tambwe wa misimu miwili iliyopita siyo huyu kwani kasi yake imepungua ndani ya uwanja kutokana na kuongezeka uzito baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Aliongeza kuwa anataka kuwa na washambuliaji wenye kasi na uwezo wa kufunga mabao kama alivyokuwa Kagere na hilo linawezekana kama mwenyewe akiwa tayari kubadilika. “Zamani Tambwe alikuwa ana uwezo wa kukimbia kilomita 30, sasa hivi anakimbia kilometa 10 kutokana na kasi yake kupungua na mara kadhaa nimekuwa nikimshauri kubadilika.
“Majeraha ndiyo yamesababisha kasi yake kupungua, kwani alikaa nje ya uwanja muda mrefu, hivyo uzito umeongezeka na kama anataka kubadilika kwanza alifanyie kazi hilo la kuupunguza mwili. “Umemuona yule mshambuliaji wa Simba Kagere (Meddie) kasi yake akiwa uwanjani?
Basi ndiyo ninataka kumuona Tambwe akifi kia kasi yake akiwa uwanjani sina hofu juu ya uwezo wake,” alisema Zahera.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam