×

NICKI MINAJ & LIL WAYNE… KWA MARA NYINGINE TENA! (PICHA)

Rapa wa kike Nicki Minaj amemvuta Young Money Boss ‘Lil Wayne’ kwa ajili ya kuandaa remix ya mdundo uliofikia mauzo ya Platinum (nakala zaidi ya milioni moja)  wa ‘Good Form’  ambao ni wimbo wa 12 kwenye albam yake ya Queen.

 

Nicki Minaj amethibitisha taarifa hizo katika akaunti yake ya Twitter kwa kuandika, “#GoodForm ft. @LilTunechi 11|27

Good Form Remix imefanywa na prodyuza Mike Will Made It na inategemewa kuingia sokoni  Jumanne Novemba 27 mwaka huu.