×

MASHABIKI WAMTAKA MARIAH CAREY KUFANYA HILI… (VIDEO)

Mwanadada Mariah Carey anayefanya vizuri hivi sasa na albam yake ya mwaka huu ‘Caution’, ametakiwa na mashabiki kufanya kolabo rapa wa kike, Cardi B.

 

Juzi (Jumatatu) Novemba  19 akiwa katika kipindi cha “Watch What Happens Live kinachoendeshwa na Andy Cohen, aliulizwa swali ambalo linahusiana na kushirikiana na Cardi B.

 

Mariah alijibu kwa kusema,“Ntapenda kama hilo litatokea, na wimbo mliokuwa mkiucheza hapa studio wa ‘A No No,’ ule wimbo halisi yake ni wa Lil Kim, tunampenda Kim, ninaamini wote watatu tutafanya kolabo. Mambo siku hizi yanafanyika haraka sana kwa hiyo huwezi kujua” alimaliza Mariah Carey

 

TAZAMA MAHOJIANO HAPA

 

‘A No No,’ ni wimbo wa Mariah Carey ambao unapatikana kwenye albam ya Caution lakini ni wimbo halisi wa rapa wa kike Lil Kim akiwa amemshirikisha B.I.G na Lil Cease uliotoka mwaka 1997.