TIMU ya masoko ya Global Publishers Ltd ikiongozwa na Anthony Adamu, jana Jumatano, Novemba 28, 2018, iliendelea na promosheni yake kabambe ya gazeti namba moja la michezo Tanzania, Champion Jumatano, huku ikiwapa mashabiki wa soka na wasomaji wa magazeti ya Global Publishers zawadi kemkem.
Katika promosheni hiyo iliyofanyika nje ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, uliyopo maeneo ya Temeke, Global Publishers kupitia gazeti la Championi, ilichezesha droo maalum ambayo iliwawezesha wapenzi wa soka kujishindia tiketi ya kushuhudia mpambano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kati ya Mabingwa wa Tanzania Simba SC na mabingwa wa Swaziland, Mbabane Swallows.
Katika droo hiyo, wasomaji walichangamkia Championi kwa kununua na kujaza kuponi kisha kuzikusanya ambapo maofisa masoko wa Global Publishers walichezesha droo hiyo na washindi kukabidhiwa tiketi zao za mechi papohapo na kuingia kushuhudia mtanange huo.
Katika mchezo huo, Simba waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 ambayo yalifungwa na John Bocco (mawili), Medie Kagere na Clatous Chama.
Wasomaji wameendelea kuipongeza kampuni ya Global Publishers kwa kuwajali wasomaji wake ambao kila kukicha wamekuwa wakinufaika kwa zawadi mbalimbali zikiwemo nyumba ambazo zimetolewa mfululizo kwa miaka miwili iliyopita, vyombo vya maakuli, pikipiki, jezi, T-shirt, ving’amuzi na zawadi nyingine kibao.
Kwa upande wao, wasomaji hao wakiwakilishwa na Juma Kidela walisema wataendelea kusoma magazeti ya Global Publishers ambayo ni Amani, Uwazi, Championi, Ijumaa, Risasi na Sport Xtra na kuwashauri wengine kununua magazeti hayo ili kujitengenezea nafasi ya kujishindia zawadi zaidi zitolewazo na Global kupitia magazeti yake.
Na Mussa Mgema | Global Publishers.
Comments are closed.