
Rapa Meek Mill amefunguka kuhusiana na aliyekuwa hasimu wake, Drake, baada ya wawili hao kupatana na kushare jukwaa ndani ya Boston, kwenye kipindi cha The Cruiz toka Radio Power 106 huko Los Angeles.
Meek Mill amefunguka na kusema walikuwa na mawasiliano mazuri kwa muda wa mwaka kabla ya kushea stage. “Tulikuwa na mawasiliano mazuri karibu mwaka mzima ila tulikuwa tunasubiri muda muafaka wa kufanya hilo na ujumbe tuliokuwa tunataka tuutoe kwa watu ni upendo na kujenga madaraja (uhusiano mzuri) na si kuharibu. Tunaona baadhi ya madaraja yanavunjika katika muziki wa Hip Hop kila mtu anafanya vitu mpaka wanafikia mbali na mwisho wa siku inakuwa ngumu kupatana. Kwa hiyo hicho ni kitu cha ushirikiano tulichofanya na uvunjifu wetu umejenga amani na umetufanya tuwe na nguvu”alifunguka Meek Mill
ITAZAME INTERVIEW HAPO CHINI SWALI LA DRAKE LINAANZIA DK 5:06
Meek Mill ameachia albam yake mpya, ‘Championships’ leo November 30 ambapo wimbo namba 9 wameufanya na Drake, unaitwa ‘Going Bad’.
ISIKILIZE ‘GOING BAD‘ HAPA
Unaweza kuipata na kuisikiliza album mpya ya Meek Mill, ‘Championships’ katika Platfom za muziki kama iTunes, Spotify, Tidal, Amazone na kwingineko.