
MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Meshack Daniel (22) ameshinda Sh milioni 226.8 za Perfect 12 za Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet.
Mkurugenzi Mkuu wa M-Bet Tanzania, Dhiresh Kaba alimkabidhi mfano wa hundi mshindi huyo mwenye umri mdogo kuliko wote tokea kuanza kwa mwaka huu.
Meshack ni mshindi wa 18 kwa mwaka huu wa droo ya Perfect 12 kwa mujibu wa Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi.
Mushi alisema kuwa Meshack ambaye ni shabiki wa timu ya Simba na Manchester United, amekwisha kabidhiwa fedha zake katika hafla fupi iliyofanyika jana kwenye hotel ya Coral Beach ya jijini Dar es Salaam.
“M-Bet ni nyumba ya mabingwa na Meshack amejiunga tena na nyumba ya mabingwa kwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitabili maisha yake, tunawaomba Watanzania kucheza michezo ya M-Bet ili kuweza kushinda kiasi kikubwa cha fedha na kuanza maisha mapya,” alisema Mushi.
Kwa upande wake, Meshack ambaye anasoma shahada ya Elimu (Bachelor of Education) alisema kuwa hakuamini kama atakabidhiwa fedha zake na kujua kuwa ushindi huo ni kiinimacho.
“Leo ndiyo nimeamini kuwa nimeshinda kiukweli baada ya kukabidhiwa fedha zangu, wakati nakuja, Dar, sikuwaambia hata wazazi wangu kwani wangenizuia kuja kutokana na mambo yaliyosambaa siku hizi ya kitapeli,” alisema Meshack.
Mshindi huyo ambaye pia ni shabiki wa timu za Barcelona, Juventus na Bayern Munich alisema kuwa imani yake na M-Bet imeongezeka na hataacha kubashiri pamoja na kushinda kiasi kikubwa cha fedha.
Alisema kuwa hatakuwa na papara kwa kushinda fedha hizo na kuwashirikisha ndugu zake katika kupanga matumizi ikiwa pamoja na kuwekeza.