×

Wagonjwa wa Corona Walazimisha Kuondoka Amana Hospital

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amethibitisha kuwa kuna baadhi ya wagonjwa walioathirika wa virusi vya Corona waliokuwa kwenye kituo maalum katika Hospitali ya Amana walikuwa wakilazimisha kuondoka na kurudi makwao wakidai wanajisikia vizuri.
Mjema amesema hayo leo Alhamisi, Aprili 23, 2020, baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa kuna baadhi ya wagonjwa hao wanadaiwa kuacha matibabu na kutoroka kwa kukimbia kisha kupanda daladala na kutokomea kusikojulikana.

“Bado hatuna taarifa ya wagonjwa waliotoroka katika Hospitali ya Amana na kupanda daladala kurejea makwao, ngoja tuifuatilie ila tunachojua ni kwamba walikuwa wanasema wanataka kurudi nyumbani, walikuwa wanatishia tu.

 

“Wagonjwa hao walikuwa wanasema wao hawaumwi sana na walikuwa wanaomba waruhusiwe.  Kumbuka ukifika pale kama unashukiwa umeambukizwa ni lazima ukae kidogo uangaliwe, sasa wao walikuwa hawataki kukaa na kutaka waondoke,” amesema Mjema.

Leave a Comment