×

Adondoka na Kufariki Papo Hapo Mwenge, Kisa Chake Utata! – VIDEO

KIFO Hakina Huruma! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kijana mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake au sura yake kudondoka na kufariki dunia maeneo ya mwenge jijini Dar es Salaam huku chanzo rasmi cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika.

Global TV imefika eneo la tukio na kuzungumza na mashuhuda wa tukio hilo ambao wamesema walimuona kijana huyo akiwa anatembea huku ana yumbayumba mithili ya mlevi na baadaye wakashangaa kuona ameanguka na kuzimika huku akitoa mapovu mdomoni na walipomsogelea wakagundua kuwa ameshapoteza maisha.