The House of Favourite Newspapers

NMB Yatoa Mfungaji Bora Mashindano Ya Kikapu

Nyota wa kikapu wa kikosi cha Benki ya NMB, Kaikai Leka (kushoto) akikabidhiwa tuzo na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori.

NYOTA wa kikapu wa kikosi cha Benki ya NMB, Kaikai Leka, ameibuka Mfungaji Bora (BestScorer) wa Ligi ya Kikapu kwa Taasisi za Fedha (BankersBasketball League BBL 2018/19), baada ya kufunga pointi 160 katika mechi za michuano hiyo iliyofikia tamati jana, jijini Dar es Salaam.

Katika fainali ya kukata na shoka jana kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, Benki ya DTB iliibuka mshindi baada ya kuifunga NMB kwa pointi 90-73, huku Leka akifunga zaidi ya nusu ya pointi zao hivyo kutangazwa Mfungaji Bora akifuatiwa na AcramMajid wa DTB, aliyefunga pointi 129.

Nahodha wa timu ya NMB Danford Kisinda akikabidhiwa Kombe la Mshindi wa pili wa mashindano hayo.

Leka alizawadiwa Tuzo ya Mfungaji Bora, kama ilivyokuwa kwa Mchezaji Bora (MVP) Leonard Benedict wa DTB, Beki Bora Frank Mwemezi wa DTB na kinara wa kufunga pointi tatu kwa mtupo mmoja (LeadingThreePointer), AcramMajid aliyefanya hivyo mara 13 katika michuano yote.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi na kufunga mashindano, Mratibu wa BBL 2018/19, Gozbert Boniface, alizipongeza timu sita zilizoshiriki michuano hiyo kwa upande wa mpira wa kikapu na kuzitaka kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao, utakaoanza baadaye mwaka huu.

“Tunaipongeza DTB kwa kutwaa taji, lakini pia kwa NMB kwa kutwaa medali za fedha za ushindi wa pili na pia kwa kutoa Mfungaji Bora wa michuano hii, iliyoshirikisha mabenki sita ya NMB, DTB, Azania, CRDB, TADB na NBC,” alisema Boniface wakati akitoa neno la shukrani.


Kwa upende wake, Mgeni Rasmi wa fainali hiyo, Juma Kimori, ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, aliwapongeza waratibu kwa wazo zuri la kuanzisha michuano hiyo, iliyoimarisha mahusiano baina ya taasisi za kifedha nchini, huku akiwapongeza mabingwa na washindi wa pili.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.