×

BARUA NZITO: JIDE, Umejiangusha Mwishoni Mwa MARATHON!

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura A.K.A Lady Jaydee hivi karibuni alizua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha ambazo siyo za kimaadili katika mtandao wake wa kijamii Instagram.

Kufuatia hali hiyo, Global Tv kupitia kwa Joseph Shaluwa amemwandikia barua nzito mwanamuziki huyo kuhusiana na tukio hilo ambalo limeonekana kumshushia heshima yake katika jamii.