×

Kibonde aagwa na mamia ya watu kwao Mbezi-Dar

Jeneza lililo na mwili wa Marehemu Kibonde likiwa nyumbani kwao Mbezi Afrikana- Dar, tayari kwa kuagwa.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga (katikati), akiongoza safu ya Wafanyakazi wa kituo hicho kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Kibonde, Nyumbani kwao Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam.
Mama wa Marehemu Kibonde (katikati) akifarijiwa na mumewe mzee Kibonde na dada yake Kibonde kabla ya shughuli ya kuuaga mwili wa mtoto wao kuanza nyumbani kwao Mbezi Afrikana.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu kibonde wakisubiria kuanza kwa zoezi la kuuaga mwili wake nyumbani kwa Mbezi Afrikana.
Baadhi ya ndugu na Wafanyakzi wa Clouds Media, wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Kibonde tayari kwa shughuli ya kuuga kabla ya kwenda kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akiwasili kuanga mwili wa Marehemu Kibonde nyumbani kwao Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya ndugu Jamaa na Wafanyakazi wenzake na marehemu Kibonde wakiwa wameketi tayari kwa kungojea shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kibonde.
Gari lilokuwa limebeba mwili wa marehemu Kibonde, likiondoka nyumbani kwao Mbezi Afrikana tayari kwa kuelekea kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuustili.
Gari lilokuwa limebeba mwili wa marehemu Kibonde (katikati), likiondoka nyumbani kwao Mbezi Afrikana tayari kwa kuelekea kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuustili.
Gari lilokuwa limebeba mwili wa marehemu Kibonde, likiwasili kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuustili.

HATIMAYE mwili wa Marehemu Ephraim Kibonde, umeagwa nyumbani kwao Mbezi Afrikana  na baadaye kwenda kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku mamia ya ndugu jamaa na Wafanyakazi wenzake kutoka Clouds Media Group wakishiriki kwenye shughuli hiyo sambamba na Wasanii maarufu na viongozi mbalimbali wa Serikali.

 

Shughuli ya kuuga mwili huo ilianza majira ya saa 7:00 mchana na baada ya kukamilika watu wote walipanda katika magari yao na kuongozana na msafara uliyokuwa umebeba jeneza lenye mwili wa marehemu kuelekea katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, tayari kwa kuhitimisha shughuli hiyo ya maziko.

 

Viongozi waliojitokeza katika zoezi la kuuga mwili huo ni Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye alikuwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Paul Makonda na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa sambamba na Waziri wa Madini Dotto Biteko pamoja na Waziri wa Utarii Dkt. Hamisi Kigwangala pamoja na Mbunge wa Mikumi Joseph Mbilinyi ‘Profesa Jay’.

 

Kwa upande wa Wasanii waliojitokeza kuuga mwili huo ni Weusi waliongozwa na Joh Makini, Nikki wa pili na Lord Eyes, wengine ni Madee, Dogo Janja, Vanessa Mdee, Lulu Diva, Banana Zoro, Jacqueline Wolper, Mpoki,  Steve Nyerere na watangazaji mbalimbali kutoka kwenye vituo kadhaa vya redio na TV wakiongozwa na Mauld Kitenge.

HABARI/PICHA; MUSA MATEJA | GPL