Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli bado anaendelea na ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Ruvuma ikiwa leo ni siku ya nne, ambapo amezindua kiwanda cha kuchakata mahindi kambi ya jeshi la kujenga Taifa Mlale.
Rais Magufuli amesema;
“Sifahamu kwanini Majeshi mengine hawaigi, sio kwamba hawafanyi ila Jeshi la Wananchi na JKT wakiambiwa tu spidi yao ni kubwa sana, hata ninapoangalia kwenye uteuzi jina linakuja la Mwanajeshi huwa nateua tu. Nawapongeza JKT Mlale kwa kuanzisha Kiwanda cha Mahindi, leo nimefurahi sana hata yale maelezo yaliyotolewa yako ‘competent’, kilichonifurahisha zaidi JKT wakiambiwa kitu wanafanya kwa kasi.
“Vijana wengi wanaomaliza JKT wananidhamu na wameiva kwelikweli, nilishatoa maagizo kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama inapofikia wakati wa kuajiri wa wasihangaike kutafuta waje kuangalia JKT. Wanaoingia JKT wana elimu zote, ndiyo maana narudia kila inapotokea nafasi mahali pa kuangalia ni JKT, na hii itapunguza upendeleo kama ni ndugu yako mwambie aende JKT akahenye kwanza
“Tunasheria ya ‘procurement’ kila kazi inatakiwa kutangazwa lakini kuna kipengele cha kazi ambayo ni emmergency, daraja likikatika sio lazima utangaze, mutumie emmergency kuwaweka wanajeshi, sijasema tenda isitangazwe ila inapotokea mchomokee. Niwaombe msiende kubadilisha kwa sababu waandishi habari mnajua kubadilisha, ‘Magufuli asema kazi zote ni wanajeshi’ sijasema hivyo nimesema kazi za ’emmergency’.
“Kwa Wizara ya Viwanda, vilivyobinafsisha na havifanyi ka, hata kama walivyovichukua ni Mawaziri vichukueni na wakikataa wapelekeni mahakamani na mtawapeleka kwa uhujumu uchumi. Mahindi katika Mkoa wa Ruvuma yanatumika kama chakula lakini kama zao la biashara, changamoto zipo na Serikali inashughulikia, msiyauze mahindi kwa bei ya kutupa
“Jirani kuna shamba la kahawa zuri sana, nikajiuliza sisi tumeshindwaje kuwatumia wafungwa kulima kahawa, au kahawa ikilimwa na Mfungwa inakauka. Nimeeleza kwenye Magereza Dar es Salaam wafungwa wamejaa lakini Magereza ya huku wafungwa ni wachache, na mashamba yapo lakini wako wafungwa wanastarehe kule mjini.
“Tumepanua viwanja vya ndege 11 tunataka ndege ziende kila mahali ikiwamo hapa Songea ambapo tumetenga jumla ya Bilioni 39 kukarabati kiwanja cha hapa Songea na Mkandarasi ameshapatikana. Mafanikio tunayoyapata kwa kasi kubwa wengine hawafurahi, wanapoacha kufurahi wanatumia mbinu nyingi saa nyingine za kuwachonganisha, wamekosa pakushika,” amesema Magufuli.