×

Wasomaji Kigamboni: Betika Limekuja Wakati Muafaka – Video

TIMU ya maofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti la Betika, imetia maguu maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam na kukutana na lundo la wasomaji wakiwa wanalisoma gazeti hilo.

Wasomaji hao walipoulizwa juu ya gazeti hilo, walionekana kulifahamu vilivyo kwani wameanza kulifuatilia tangu toleo la kwanza lilivyotoka Februari, mwaka huu.

Wakilizungumzia gazeti hilo ambalo hutoka kila Jumatano, wasomaji hao walisema limekuwa msaada mkubwa kwao katika suala zima la kubeti.

“Betika ni bonge la gazeti, huwa nasoma magazeti mengi ya michezo na kujua habari nyingi za michezo, lakini zamani kabla ya ujio wa gazeti hili, nilikuwa napata shida sana linapokuja suala la kubeti.

“Ukilisoma Betika, unapata maujanja ya kubeti kwa sababu kuna uchambuzi wa mechi mbalimbali unaoweza kukufanya uweke mkeka wako vizuri na kushinda,” alisema mmoja wa wasomaji wa gazeti hilo.

Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, aliendelea kusisitiza kwamba bado kuna nafasi ya watangazaji kuleta matangazo yao ili kutangaza na gazeti hilo.

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

“Pia bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu,” alisema Mgema.

Betika ambalo ni mahususi kwa kubeti, lina kurasa 20 za rangi ambapo mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya na hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18.

MWANDISHI WETU