×

Betika  Kugawiwa Bure Katika Maboksi Maalum Dar

Msomaji wa gazeti la Betika akiwa amelichukua katika sanduku (box) maalum eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Mwanadada akilichukua gazeti la Betika eneo la stendi ya daladala ya Makumbusho.
Mmoja wa wasambazaji wa masanduku ya Betika kutoka Kampuni ya Global Publishers Ltd, akipozi katika eneo la kibanda cha kubeti eneo la Mabibo.
Msomaji akichukua gazeti la Betika.
Mkazi wa Dar akichukua Betika. 
Mdau wa Betika akilichangamkia jijini Dar.
Mmoja wa wasambazaji wa Global akiwa tayari kuhudumia wateja wa Betika.
Wasambazaji wa Gazeti la betika wakiwa katika picha ya pamoja na moja ya ma-box ya gazeti hilo.
Taswira kamili ya sanduku maalum la Betika.

 

LIKIWA na takribani miezi miwili mtaani, Gazeti la Betika limezidi kutikisa kila kona  nchini  ambapoleo Aprili 17 limemwaga masanduku (box) maalum kwa ajili ya wasomaji wa gazeti hilo kwa ajili ya kulipata bure kila linapotoka.

 

Gazeti hilo ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 kwenda juu.

 

Timu ya maofisa masoko wa Global Publishers imeingia mtaani leo Jumatano na kusambaza masanduku hay katika maeneo maalum kwa lengo la kuwarahisishia wasomaji wa Betika waweze kulipata kwa urahisi.

Akizungumza juu ya kusambaza ma-box hayo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Ofisa Masoko wa Global, Mussa Mgema, alisema:

“Kwa kuboresha zaidi katika Jiji la Dar es Salaam, tumesambaza maboksi maalum ambayo ndani yake kuna nakala nyingi za gazeti hilo ambapo msomaji anatakiwa kuchukua bure na kujipatia uhondo.

 

Betika lina kurasa 20 za rangi ambapo mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.