The House of Favourite Newspapers

MIMBA YA TANASHA FAMILIA YACHEKELEA

DAR ES SALAAM: Mpenzi wa sasa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ameibua gumzo kufuatia muonekano wake wa sasa unaomuonesha akiwa na dalili zote za kuwa mjamzito. 

 

Hayo yameibuka baada ya hivi karibuni mwanadada huyo raia wa Kenya kutupia picha mtandaoni ambayo iliwafanya wajuvi wa mambo kuikagua vilivyo na kuhitimisha kuwa ni mjamzito.

 

“Kitumbo bado hakijatoka kivile lakini ana kila dalili kwamba amenasa mimba. Ukitaka kujua kwamba kweli ana ujauzito angalia mashavu yake, pua na hata sehemu ya kifuani, unaona kabisa ana kitu tumboni,” alisema Fatuma Kija wa Sinza jijini Dar baada ya kuiona picha hiyo.

 

Aidha, picha hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya waliokomenti waliishia kumpongeza kwa kukubali kuzaa na Mondi huku wengine wakimtahadharisha kuwa, asipoangalia yatamkuta yaliyowakuta waliomtangulia (Zari na Mobeto).

 

“Anabeba mimba kabla ya ndoa, asubirie kutoswa tu,” alikomenti mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Double J kwenye mtandao wa Instagram.  Mwingine akaandika: “Waoo shemeji langu la nguvu, zaa mama… zaa umzalie Simba, pesa ya kukutunzia ipo.”

 

Huko huko Insta baada ya Diamond kuona watu wakimpongeza mpenzi wake, naye alikomenti kwenye picha hiyo akisema: “Kileee, nakiona kwa mbali (akimaanisha anakiona kibendi kwa mbali).

FAMILIA YA MONDI YACHEKELEA

Akizungumza na Amani kuhusu madai hayo kuwa wifi yake (Tanasha) ni mjamzito, Asma Khan (Dada wa Diamond) alisema: “Jamani ni kitu cha furaha sana kwetu, kama anayo si mtaona? Sisi tunafurahia uhusiano uliopo kati yao na wakituletea mtoto mwingine furaha itaongezeka maana tunapenda watoto na bahati nzuri hata pesa ya kuwalelea ipo.”

 

Naye baba wa Diamond, Abdul Juma alipozungumza na gazeti hili kuhusu ya madai mkwe wake Tanasha kuwa mjamzito alisema: “Hizo taarifa zimenifurahisha sana, kama amenasa azae tu maana namkubali kwa kweli. Ila isije ikawa ni maneno ya watu tu.”

 

Tanasha amekuwa kwenye uhusiano na Diamond kwa kipindi cha miezi kadhaa huku kukiwa na taarifa za wawili hao kuwa kwenye mpango ya kuingia kwenye maisha ya ndoa huku hilo la mimba likiwa si Diamond wala Tanasha aliyeliweka wazi.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Comments are closed.