×

Nandy, Mobeto kunani tena?

WAKATI watu wako bize kuwaza pesa hii imekuwa tofauti kwa warembo wawili wanaofanya vizuri kwenye gemu ya muziki wa Bongo Fleva na filamu! Unaambiwa mwanadada Faustina Charles ‘Nandy’ ameingia katika bifu kubwa na msanii mwenzake, Hamisa Mobeto.  Kwa mujibu wa vyanzo, wawili hao wamefikia hadi hatua ya kublokiana katika mitandao ya kijamii huku sababu ikitajwa ni picha aliyowahi kupiga Nandy akiwa na Diamond.

“Unajua kuna kipindi Hamisa alikuwa ametoka kuachana na Diamond, wakati huohuo picha ikasambaa Nandy akiwa naye kuanzia hapo wakawa hawasemeshani wala kusapostiana,” kilisema chanzo. Mikito Nusunusu lilianza kwa kumtafuta Hamisa anayebamba na Ngoma ya Sensema na kumuuliza madai haya ambapo aliongea kwa kifupi tu kwamba hana muda wa kumzungumzia Nandy.

“Hiyo ishu haina umuhimu kwa sasa, aniblock asiniblock mimi hainipunguzii chochote ninachoangalia ni maisha yangu na familia yangu basi, so (kwa hiyo) ni bora tukazungumzia mambo ya maana mfano kama sasa hivi nimetoa wimbo wangu mpya wa Sensema hivyo nahitaji sapoti.

Baada ya kuzungumza na Hamisa, Mikito Nusunusu lilimgeukia na Nandy ambapo naye alisema yupo bize na kazi hivyo hawezi kuzungumzia vitu ambavyo havina faida kwake “(Anacheka) Kwani yeye kasema ana bifu na mimi? Bwana ee sikia mimi nipo bize na kazi zangu sasa hivi nawaza nifanye nini ili nizidi kuwaburudisha mashabiki zangu,” alisema Nandy.

STORI: MEMORISE RICHARD