×

TBL Yazindua Promosheni Ya Kizibo Pesa, Watoa Punguzo La Bei -Video

Meneja wa bia ya Safari Lager, Pamela Kikuli alipokuwa akiongea na wanahabari Kinondoni Morocco Dar, leo.

Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa bia nchini, Tanzania Breweries Limited (TBL) leo imezindua promosheni iitwayo Kizibo Pesa ambapo kizibo cha bia ya Safari Lager ya mililita 500 kitakuwa na thamani ya fedha hadi Sh.200 ambazo watumiaji watazitumia kujipatia punguzo wakati wa kununua bia nyingine ya aina hiyo.

Pamela akizindua promosheni hiyo.

Akiongea na waandishi kwenye mkutano uliofanyika Kinondoni Morocco, Dar, leo Meneja wa bia hiyo, Pamela Kikuli amewaambia kuwa kwa miaka kadhaa sasa TBL imezawadiwa tuzo mbalimbali za dhahabu kupitia zao za vinywaji wanavyozalisha.

Amesema sasa kwa tuzo ya dhahabu waliyoipata hivi karibuni wameona umuhimu wa kusherehekea mafanikio hayo na wateja wao wa dhati.



1

2.

3.Akionesha tuzo waliyoshinda.

4.Wanahabari kazini.

5.Burudani zikiendelea wakati wa hafla hiyo.

6.Mfano wa kizibo cha promosheni hiyo.

HABARI: NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS

GPL

Leave a Comment