×

Bilionea Ali Mufuruki Amefariki Dunia

 

Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group ambaye aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, Ali Mufuruki (60), amefariki  Dunia jana Desemba 7, 2019 akiwa Afrika Kusini akipatiwa matibabu.

 

Mufuruki ambaye ni mwenyekiti mwanzilishi wa Jukwaa la maofisa watendaji wakuu wa  kampuni (Ceo roundtable) amekutwa na umauti akiwa na familia yake.

 

Mufuruki ni kati ya matajiri wakubwa 10 wa Tanzania akiwa ni mmiliki wa Kampuni ya Infotech Investment Group Limited na maduka ya Wolworth.

 

Oktoba 18, 2019 Mufuruki alijiuzulu nafasi yake ya  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania ili kupata muda zaidi wa kuendelea na biashara zake.

Leave a Comment