MWILI wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco umeagwa leo baada ya kufanyiwa ibada katika kanisa la KKKT Kimara-Temboni jijini Dar es Salaam.
Seth ambaye alifariki juzi Jumamosi, Desemba 7, 2019 atazikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.