×

Mobeto Aamsha Yaliyolala Wasafi

DAR ES SALAAM: Mambo yametaradad! Unaambiwa mrembo Hamisa Mobeto amesababisha tukio baada ya kupostiwa kwenye ukarasa wa Wasafi TV, Instagram.

Wasafi TV walimposti Mobeto juzi, Jumanne kwenye ukurasa wao na kusindikiza na ujumbe mzito ambao kimsingi ndio uliozua balaa lililolala.

 

Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi:

“Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa mwanamitindo na mwanamuziki @ hamisamobetto akiongeza mwaka mwingine katika maisha yake, @hamisamobetto alianzia kwenye mitindo na kufanya vizuri hapa nchini na kisha baadae kuhamia kwenye upande wa uimbaji na kutoa ngoma tofauti akifanya kazi na producers pamoja na wasanii tofauti.

 

Happy Birthday @ hamisamobetto.”

Sasa basi, baada ya ujumbe huo kupostiwa, wananzengo waliliamsha dude kama lote kumhusu bosi wa Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

 

“Haiwezekani hawa wampambe namna hii, lazima kuna maelekezo kutoka kwa bosi wao Diamond ambaye ni mzazi mwenziye Mobeto,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.

Mdau mwingine alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa, mrembo wa sasa wa Mondi, Tanasha Donna anatakiwa kuwa makini maana jamaa huyo haaminiki.

 

“Mh! Tanasha anatakiwa kuwa makini maana sio kwa sifa hizi, si ajabu Mondi anataka kurejesha majeshi upya.”

Hata hivyo, licha ya mashuti kuwa mengi kwenye mtandao huo, si Diamond, si Mobeto wala Tanasha walioibuka kusema lolote hadi tunakwenda mitamboni.

 

Mobeto na Mondi walikuwa kwenye uhusiano wa siri wakati ambao Mondi alikuwa kwenye uhusiano mzito na Zari.

Penzi hilo la siri liliweza kuzaa matunda kwa wawili hao kupata mtoto mmoja kabla ya kuachana na sasa Mondi yupo kwenye uhusiano na Tanasha.

Wakati huohuo, juzikati Mobeto ametangaza kuwa yupo singo kwa takriban mwaka mzima.

Stori: Neema Adrian, Amani

Mshtuko Dar! Vijana Wachinja, Wala Nyama Mbichi ya Paka

 

Leave a Comment