
KLABU ya Yanga imefanikiwa kumrejesha nchini beki wake kisiki Lamine Moro kuelekea mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba ambao utapigwa January 04, 2020 kwenye uwanja wa Taifa.
Beki huyo raia wa Ghana aliondoka wiki iliyopita muda mfupi baada ya kuandika barua ya kuvunja mkataba wake kufuatia kukosa mishahara kwa miezi miwili.
Inaelezwa mabosi wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga waliingia kati sakati lake ambapo walimleta nchini Meneja wake kwa ajili ya mazungumzo ambayo mwafaka umefikiwa kwa pande zote mbili.
Kulikuwa na taarifa kuwa klabu ya Simba ilikuwa ikimnyemelea beki huyo ambaye walishindwa kumsajili mapema mwaka huu licha ya kumfanyia majaribio.