×

Unatafuta Shule Ya Mwanao? St. Mary’s Ndiyo Jibu Lako

 

ZIMEBAKI siku chache kabla ya kuumaliza mwaka 2019 na kuingia 2020! Kwa kawaida, mwezi huu na Januari, ni kipindi ambacho wazazi huhangaika huku na kule kuwatafutia shule watoto wao na kama na wewe ni miongoni mwao na unajali ubora wa elimu na mazingira ya shule, basi Shule za St. Mary’s ndiyo jibu lako.

 

Ipo wazi kwamba, Shule za St. Mary’s ni miongoni mwa shule za mwanzo kabisa nchini kuanza kufundisha kwa kufuata mtaala wa Kingereza (English Medium) zikiwa zimeanza mwaka 1998 na kwa miaka mingi zimeendelea kuwa kinara kwa utoaji wa elimu bora ambayo humuandaa mtoto kukabiliana na changamoto za kimaisha hapo baadaye.

 

Katika msimu huu wa masomo, Shule za St. Mary’s zinakutangazia wewe mzazi ofa kabambe itakayomuwezesha mwanao kupata elimu bora kwa ada nafuu huku pia mzazi akiwa na nafasi ya kulipa kwa awamu ili kupunguza mzigo wa karo!

 

Unachotakiwa kufanya, ni kutembelea moja kati ya Shule za St. Mary’s iliyo karibu na wewe ambapo utapewa utaratibu maalum wa namna ya kumwandikisha mwanao kwa urahisi kabisa.

 

Shule za St. Mary’s zimesambaa karibu nchi nzima; kuna St. Mary’s ya Tabata, St. Mary’s ya Mbezi- Beach na Mbagala zote za jijini Dar es Salaam, St. Mary’s Mbeya, St. Mary’s Dodoma na St. Mary’s Ifakara na St. Mary’s Kihonda, zote za Morogoro huku malengo yakiwa ni kuwa na shule katika mikoa yote ya Tanzania.

 

Pia zipo Shule za Kenton na East Africa International School ambazo nazo pia zipo chini ya St. Mary’s, zote zikiwa zinafundisha kwa kufuata mtaala wa Kiingereza na kutoa wanafunzi bora kabisa ambao wamekuwa wakipata mafanikio makubwa kwenye elimu za juu ndani na nje ya nchi.

 

“Ubora unaotolewa kwenye shule zetu, unaanzia kwenye mazingira ya kujifunzia na kusomea. Shule zetu zina mandhari nzuri ambayo itamvutia mwanafunzi kupenda kusoma hata kama hakuwa akipenda. Tuna majengo mazuri na ya kisasa, viwanja vya michezo mbalimbali, kuna usafiri kwa wanafunzi wanaokaa maeneo ya mbali na chakula kizuri.

 

“Pia tuna walimu wazoefu ambao watahakikisha mwanao anaelewa anachofundishwa hata kama akiwa mzito kichwani! Tuna vitabu vya kila aina, tuna maabara za kisasa zikiwemo za kompyuta ili kumfanya mwanafunzi aendane na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia.

 

“Pia wanafunzi hufanya mitihani ya mara kwa mara kwa lengo la kuwaandaa vizuri na mitihani ya mwisho na kuwaondolea hofu ya mitihani ya taifa,” alisema Rose Rwakatare, mmoja wa wakurugenzi wa shule hizo.

Asilimia kubwa ya wanafunzi waliopitia kwenye shule hizi ni wahitimu wa vyuo vikuu, wengi wameajiriwa au kujiajiri kwa mafanikio makubwa! Hiyo yote ni kwa sababu ya msingi imara ambao waliupata kutoka Shule za St. Mary’s.

 

Habari njema zaidi ni kwamba shule hizo katika msimu huu wa kuelekea msimu mpya wa masomo wa 2020, zinatoa ofa kubwa kwa wanafunzi wenye vipaji maalum, kujiunga na shule zao kwa punguzo la ada.

 

Kama wewe ni mzazi na una uhakika mwanao ana kipaji cha kitaaluma, changamkia ofa hii kwa kwenda katika shule yoyote ya St. Marys iliyo karibu nawe, mwanao atapimwa uwezo wake wa kitaaluma na akifuzu vigezo, basi utapata ofa ya punguzo kubwa la ada!

 

Namna ya kuwasiliana nao, unaweza kupiga namba za simu zifuatazo kulingana na shule unayoitaka ambayo itakuwa rahisi kwako kumpeleka mwanao;

 

St. Mary’s Mbeya (0713435776), St. Mary’s Dodoma (0718088834), St. Mary’s Morogoro (0713212911), St. Mary’s Mbezi – Beach, Dar es Salaam (0654994193), St. Mary’s Mbagala, Dar es Salaam (0713427641), St. Mary’s Tabata (0754428183) na East Africa International School (0713217898).

 

Pia unaweza kuwatembelea kwenye mtandao wa Instagram kwa anuani ya @st.marys_ schooltz.

 

MAKALA: MWANDISHI WETU, DAR

 

MTOTO MDOGO ANAONGEA KINGEREZA BALAA, UTAPENDA!

Leave a Comment