The House of Favourite Newspapers

Wema Amzulia Balaa Diamond Platnumz

0

MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mrembo kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Wema Sepetu kumzulia balaa zilipendwa wake ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Amani linakupa habari kamili.

 

Wema amejikuta akimzulia balaa hilo msanii huyo ikiwa ni baada ya hivi karibuni, Diamond kujirudi kwa maadui zake ambapo amekuwa akiweka picha zao katika ukurasa wake wa Instagram akiwaelezea kwamba watakuwa kwenye shoo yake ya kuadhimisha miaka 10 kwenye muziki itakayofanyika Kigoma, Desemba 31, mwaka huu.

 

Kutokana na zoezi hilo la Diamond ambalo linaonekana ni endelevu mpaka siku ya shoo ifike, lilizua gumzo la aina yake ambapo baadhi walimpongeza huku wengine wakimponda.

WEMA AMZULIA BALAA

Mjadala uliendelea ambapo balaa lilizuka baada ya mashabiki kutoona picha ya Wema ambapo walimchamba Diamond vilivyo na kumuuliza kulikoni kutomposti wakati ndiye mwanamke mwenye mchango mkubwa sana kwenye muziki wake.

 

“Wema ana mchango mkubwa sana kwa Diamond maana ndiye aliyemfanya mpaka akajulikana kwa watu yaani akawa staa lakini katika watu aliowaposti kwenye ukurasa wake hajamuweka kwamba naye atakuwepo.

“Kwa jinsi alivyomsaidia mpaka akafika hapo alipo, Diamond alitakiwa kumwalika na kumposti Wema kama alivyofanya kwa hao wengine hata kama wamekosana kiasi gani, ni kosa gani hilo kubwa asisamehe na kuendelea na maisha kama kawaida,” aliandika mmoja wa wafuasi wa Diamond.

 

AUNT ACHOCHEA

Kutokana na kitendo hicho, msanii wa filamu Aunt Ezekiel, alionekana kama amechochea ikiwa ni baada ya Diamond kumposti na kusema atakuwepo siku hiyo.

Hapo sasa mashabiki wenye mapenzi na Wema walianza kumtolea maneno wakimuhoji je, Aunt ni muhimu kuliko Wema ambaye alimtoa chini kabisa na kumuweka juu alipo sasa.

 

WEMA ANASEMAJE?

Amani lilimtafuta Wema ili kujua anazungumziaje kitendo hicho cha Diamond kutompa mwaliko lakini simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Leave A Reply