Kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa Shule za Zam Zam, Rashid Bura Jumatano Desemba 25, 2019 ofisini kwake eneo la Majani ya chai karibu na Nyerere square, Dodom Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya kilichosababisha kifo cha mkurungenzi huyo ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto Katika Taarifa yake aliyoitoa leo 27/12/2019 amesema kifo cha mkurungenzi huyo kimesababishwa na tatizo la moyo kufeli.
Mwili wa Rashid Bura ulitarajia kuzikwa jana mchana, Alhamisi ya Desemba 26, 2019 katika makaburi ya Chamwino Dodoma.