
RAHA ya sikukuu upate zawadi! Hiyo ndiyo sababu iliyofanya Kampuni ya Azania, watengenezaji wa sabuni za King Limau na Marhaba kumwaga zawadi kibao msimu huu wa sikukuu kwa watumiaji wa sabuni hizo na wasomaji wa Magazeti ya Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Hata wewe unaweza kuwa mshindi kwani ni rahisi mno kujizolea zawadi kibao! Unachotakiwa kufanya ni kujaza kuponi maalum iliyopo kwenye ukurasa huu, na ambayo hutoka kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda na Ijumaa, kisha ijaze kwa kufuata maelekezo.

Utatakiwa kujaza jina lako kamili, namba yako ya simu, umri wako kisha utajibu swali rahisi lililopo kwenye kuponi. Baada ya hapo, chukua simu yako kisha nenda kwenye sehemu ya kutuma meseji (SMS), andika namba kubwa zinazoonekana kwenye kuponi (mfano 100100), kisha zitume kwenda namba 0753 715 779 kisha kata kuponi yako na uihifadhi kwani itahitajika wakati wa kuchukua zawadi.

“Kwa kutuma meseji, moja kwa moja unakuwa umeingia kwenye kinyang’anyiro cha kujishindia zawadi kibao katika msimu huu wa sikukuu! Zawadi zitakazokuwa zinatolewa zitakuwa ni pamoja na ndoo za sabuni, fulana, fedha taslimu na zawadi nyingine kibao,” alisema Catherine Kahabi, mratibu wa shindano hilo.
Mbali na zawadi hizo zinazotolewa msimu huu wa Sikukuu, watumiaji mbalimbali wa sabuni mpya za King Limau na Marhaba sehemu mbalimbali nchini, wameendelea kushangazwa na maajabu makubwa katika usafi yanayoletwa na sabuni hizo.

“Kazi zangu huwa zinanifanya nachafuka sana, nafanya kazi ya ufundi rangi! Kwa kipindi kirefu nilikuwa naharibu sana nguo kwa sababu sabuni za kawaida hazitakatishi kabisa.
“Ila tangu nilipozijua Marhaba na King Limau, mambo yamebadilika kabisa, nawapongeza sana watengenezaji wa hizi sabuni Salim Kidilu, fundi anayefanya kazi zake maeneo ya Tandika alimwambia mwandishi wetu wakati wa promosheni ya sabuni hizo inayoendelea mitaani.

Tofauti kabisa na sabuni nyingine za unga, King Limau na Marhaba, hazichubui kabisa mikono na hii inamuwezesha mtumiaji kufua nguo nyingi bila kuwa na hofu ya mikono yake kuharibika.
Pia kiasi kidogo cha sabuni, iinatoa povu jingi ambalo lina uwezo wa kutoa hata yale madoa sugu ambayo yameshindikana kwa sabuni nyingine za kawaida! Uzuri zaidi ni kwamba licha ya kuzitakatisha nguo zako na kuzipa mng’aro wake wa asili, King Limau na Marhaba huziacha nguo zako zikiwa zinanukia vizuri kabisa!

Namna ya kujipatia sabuni hizo, ni rahisi sana! Nenda duka lolote lililo jirani na mahali ulipo, usiseme sabuni ya unga bali sema King Limau au Marhaba Soap na muuzaji atakupatia kwa bei nafuu kabisa! Kisha baada ya hapo, nenda kaijaribu mwenyewe na utaona matokeo yake!
Kwa mawasiliano zaidi, wapigie kwa namba 0710 111 112 au watumie barua pepe kwa anuani ya email: sales@ azaniagroup.company.
Makala: Mwandishi Wetu, Ijumaa Wikienda