×

Vigogo Wawili Wanaswa na Dawa Za Kulevya Dar

Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya,  James Wilbert Kaji,  akizungumzia oparesheni inayoendelea dhidi ya madawa ya kulevya jana jijini Dar es Salaam.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imetangaza kuwanasa vigogo wawili wa biashara haramu ya dawa hizo katika oparesheni kali ya kuzitokomeza ambayo inaendelea.

 

Akizungumza na wanahabari,   Kaji amesema watuhumiwa hao ni Abuu Salehe Kimboko mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam,  na Paschal Peter Lufunga mkazi wa Bwilingu, Kibaha, mkoani Pwani, wote wakisemekana walikuwa washiriki wa biashara hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

…Akifafanua jambo.

Pia amedai amethibisha ukinara wa watuhumiwa hao kutokana na kila muuzaji aliyekamatwa alipobanwa aliwataja vigogo hao kuwa ndiyo waliomuuzia dawa hizo.

 

Akizungumzia jinsi walivyowanasa, amesema Kimboko alinaswa maeneo ya Mbagala-Zakiem, Dar, Desemba 29, 2019,  akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin gramu 400  na bastola moja yenye risasi 15.

Kamishna wa Tiba na Kinga wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Dkt. Peter Mfisi,  akifafania kuhusu tiba na kinga kwa waathirika wa dawa hizo.

Kaji alindelea kusema Lufunga alikamatwa nyumbani kwake Bwiligu akiwa na heroin gramu 133.33. ambapo wote wawili amesema wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Wanahabari akia kazini wakati wa mkutano huo.

Katika mkutano huo pia, Kaji  alisma kwa siku za hivi karibuni kesi 35, za dawa hizo zimeshatolewa uamuzi na kuteketezwa na zile ambazo zilitolewa maamuzi ambayo mamlaka hiyo haikuridhika nayo ilizikatia rufaa.

Kamishna wa Sheria wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Burhani Kishenyi (kulia), akichambua mambo ya kisheria.

(HABARI/PICHA: MWANDISHI WETU)

Leave a Comment