
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imetangaza kuwanasa vigogo wawili wa biashara haramu ya dawa hizo katika oparesheni kali ya kuzitokomeza ambayo inaendelea.
Akizungumza na wanahabari, Kaji amesema watuhumiwa hao ni Abuu Salehe Kimboko mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam, na Paschal Peter Lufunga mkazi wa Bwilingu, Kibaha, mkoani Pwani, wote wakisemekana walikuwa washiriki wa biashara hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Pia amedai amethibisha ukinara wa watuhumiwa hao kutokana na kila muuzaji aliyekamatwa alipobanwa aliwataja vigogo hao kuwa ndiyo waliomuuzia dawa hizo.
Akizungumzia jinsi walivyowanasa, amesema Kimboko alinaswa maeneo ya Mbagala-Zakiem, Dar, Desemba 29, 2019, akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin gramu 400 na bastola moja yenye risasi 15.

Kaji alindelea kusema Lufunga alikamatwa nyumbani kwake Bwiligu akiwa na heroin gramu 133.33. ambapo wote wawili amesema wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Katika mkutano huo pia, Kaji alisma kwa siku za hivi karibuni kesi 35, za dawa hizo zimeshatolewa uamuzi na kuteketezwa na zile ambazo zilitolewa maamuzi ambayo mamlaka hiyo haikuridhika nayo ilizikatia rufaa.

(HABARI/PICHA: MWANDISHI WETU)